Kilimo cha zao la nyanya ,nyanya ni mmea jamii ya tunda,linalolimwa nchini Tanzania na dunianiani kwa ujumla ndani ya nchi yetu nyanya inalimwa katika mikoa ya iringa ,Morogoro, dodoma, Pwani ,njombe ,mbeya ,arusha ,kilimanjaro .n.k. mmea huu husitawi kwa wingi hasa maeneo yenye ukanda wa joto kuliko ukanda wa baridi sana.
Nyanya kama tunda hutumika katika matumizi mbali mbali ikiwemo
1.majumbani km kiungo
2. viwandani kutengenezea chill sauce na tomatoes
3.hoteli km kiungo pia lakini husaidia katika kusafisha macho ukila km tunda.
AINA ZA NYANYA
Kuna aina zaidi ya kumi za mbegu za nyanya ndani ya nchi TANYA ,RIO GRAND,MKULIMA,MWANGA,ROMA,DUMU DUMU nje ya nchi nikimanisha jamii ya HYBRID , ANNA ,VERONICA,EDEN F1,ASSILA F1,KIRERE, SHANTI .n.k.
SOKO LENGWA
Ndani ya nchi soko la nyanya lipo kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na uzalishaji masoko makuu yanayotegemewa kwa kuuzaji ni ilala ,kariakoo, karume,kibaigwa n.k na mikoa yote isiyojikita sana ktk uzalishaji ikiwemo dodoma, singida ,mtwara,lindi, na pia masoko ya nje ya nje yapo km kenya ,uganda,kongo,zambia n.k. N.B.kuna viwanda vikubwa km dabaga na dash mkoani iringa na dash mkoani arusha waweza ingia nao mkataba wa kupeleka bidhaa mwaka mzima.
Mchanganuo wa uzalishaji ,Kwa mbegu jamii ya HYBRID hukomaa baada ya siku 70-75, kwa hekari moja huweza kutoa tenga 1000 ukihudumia vizuri ikipungua sana 800,kwa nyanya yenye ubora wa grade ya kwanza. na mbegu zetu hizi hutumia siku 90 na kwa hekari hufikisha tenga kiasi cha juu 600,kwa mantiki hiyo HYBRID ni nzuri na ina tija sana .
Makadilio ya mauzo kuweza kutambua bei au kufanya makadilio ya mauzo tuna panga kwa vipindi vitatu km ifuatavyo
1,Uzalishaji kwa wingi hapo ni ule wakati watu wengi wamezalisha hasa kuanzia mwezi wa nne mpaka saba kwa kuwa wanategemea kilimo cha mvua na hasa hii kwa maeneo mengi ya nchini yetu kwa shamba tuuze kwa 6000 tukizidisha na tenga 800 upata 4,800,000 na sokoni 15000 tutapata 12,000,000/ .
2.uzalishaji wa wastani mwezi saba mpaka nov idadi ya tenga ile ile bei ya shamba 12000tukizidisha tunapata 9,600,000.kwa bei ya sokoni 25000, tutapa 20,000,000,
3.msimu huu tuliopo uzalishaji kiasi kidogo dec-march bei ya shamba 25000 tukizidisha mara tenga 800 tunapata 20,000 .bei ya sokoni 45,000.tutapata 36,000,000. .
N.B.KWASASA SHAMBA NAUZA 30000-35000 na sokoni 50000-65000, ALIEPO JIRANI ASHUHUDIE ATAJE BEI SEHEMU ALIPO SIO MAIGIZO.
Gharama ya uendeshaji ni kiasi cha milioni mbili na nusu 2,500,000 kiasi cha juu ikiwemo mbolea ,madawa,kukodi shamba ,kununua mbegu na bomba za kupulizia dawa.
Magojwa makuu yanayoshambulia nyanya nitatoa mfano mmoja wa dawa
1.wadudu dawa zake phamarphorce au celocron.
2.mbolea za majan
SUPER GRO, BUSTA
3.Ukungu -lincolin
4.kutu -movil au defender
5.kuoza mizizi -victory.n.k
Alfan Yusuph
Inspiration for sucess
1 comments:
Nashkuru mkuu kwa taarifa.Kwa ufupi nimefurahi sana na somo lako.Unalimia maeneo(mkoa) gani hapa nchini??
Post a Comment