Tuesday, December 22, 2015

Kilimo cha NYANYA


Kilimo cha zao la nyanya ,nyanya ni  mmea jamii ya tunda,linalolimwa nchini Tanzania na dunianiani kwa ujumla ndani ya nchi yetu nyanya inalimwa katika mikoa ya iringa ,Morogoro, dodoma, Pwani ,njombe ,mbeya ,arusha ,kilimanjaro .n.k. mmea huu husitawi kwa wingi hasa maeneo yenye ukanda wa joto kuliko ukanda wa baridi sana.

Nyanya  kama tunda hutumika katika matumizi mbali mbali ikiwemo 
1.majumbani km kiungo
2. viwandani kutengenezea chill sauce na tomatoes 
3.hoteli km kiungo pia lakini husaidia katika kusafisha macho ukila km tunda.

AINA ZA NYANYA
Kuna aina zaidi ya kumi za mbegu za  nyanya ndani ya nchi TANYA ,RIO GRAND,MKULIMA,MWANGA,ROMA,DUMU DUMU nje ya nchi  nikimanisha jamii ya HYBRID , ANNA ,VERONICA,EDEN F1,ASSILA F1,KIRERE, SHANTI .n.k.

SOKO LENGWA
Ndani ya nchi soko la nyanya lipo kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na uzalishaji masoko makuu yanayotegemewa kwa kuuzaji ni ilala ,kariakoo, karume,kibaigwa n.k na mikoa yote isiyojikita sana ktk uzalishaji ikiwemo dodoma, singida ,mtwara,lindi,  na pia masoko ya nje ya nje yapo km kenya ,uganda,kongo,zambia n.k. N.B.kuna viwanda vikubwa km dabaga  na dash mkoani iringa na dash mkoani arusha waweza ingia nao mkataba wa kupeleka bidhaa mwaka mzima.

Mchanganuo wa uzalishaji ,Kwa mbegu jamii ya HYBRID hukomaa baada ya siku 70-75, kwa hekari moja huweza kutoa tenga 1000 ukihudumia vizuri ikipungua sana 800,kwa nyanya yenye ubora wa grade ya kwanza. na mbegu zetu hizi hutumia siku 90 na kwa hekari hufikisha tenga kiasi cha juu 600,kwa mantiki hiyo HYBRID ni nzuri na ina tija sana .

Makadilio ya mauzo kuweza kutambua bei au kufanya makadilio ya mauzo tuna panga kwa vipindi vitatu km ifuatavyo
1,Uzalishaji kwa wingi hapo ni ule wakati watu wengi wamezalisha hasa kuanzia mwezi wa nne mpaka saba kwa kuwa wanategemea kilimo cha mvua na hasa hii kwa maeneo mengi ya nchini yetu kwa shamba tuuze kwa 6000 tukizidisha na tenga 800 upata 4,800,000 na sokoni 15000 tutapata 12,000,000/ .

2.uzalishaji wa wastani mwezi saba mpaka nov idadi ya tenga ile ile bei ya shamba 12000tukizidisha tunapata 9,600,000.kwa bei ya sokoni 25000, tutapa 20,000,000,

3.msimu huu tuliopo uzalishaji kiasi kidogo dec-march bei ya shamba 25000 tukizidisha mara tenga 800 tunapata 20,000 .bei ya sokoni 45,000.tutapata 36,000,000. .
N.B.KWASASA SHAMBA NAUZA 30000-35000 na sokoni 50000-65000, ALIEPO JIRANI ASHUHUDIE ATAJE BEI SEHEMU ALIPO SIO MAIGIZO.

Gharama ya uendeshaji ni kiasi cha milioni mbili na nusu 2,500,000 kiasi cha juu ikiwemo mbolea ,madawa,kukodi shamba ,kununua mbegu na bomba za kupulizia dawa.

Magojwa makuu yanayoshambulia nyanya nitatoa mfano mmoja wa dawa
1.wadudu dawa zake phamarphorce au celocron.
2.mbolea za majan
SUPER GRO, BUSTA
3.Ukungu -lincolin
4.kutu -movil au defender
5.kuoza mizizi -victory.n.k 

Alfan Yusuph 
Inspiration for sucess

Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko


Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).

Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

N:B
Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.


Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi
Hatua  ya kwanza
Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki.

Hatua ya pili
Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke.

Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa.

Hatua ya tatu
Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi.

Njia ya pili
Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C

Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo.

Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya kasha la mbao lilotangulizwa karatasi nyembamba la plastiki subiri saa 3 na sawazisha sabuni kwa rula au kitu kingine kilicho nyooka huku ukigandamiza juu, ipanguse iwe laini kwa kutumia kitamba kilicho lowanishwa.

Katakata sabuni vipande kwa kipimo cha kuuza iweke ikauke katika sehemu yenye kivuli kwa muda wa majuma 8 hadi 12 mfano- ndani ya chumba kwenye sakafu iliyotandikwa kasha la karatasi nene.

Kwa hisani ya Darasa huru

Kilimo cha matikiti maji (watermelon): Ushauri na Masoko


Matikiti maji aina ya  Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna ukiongeza na  siku 3-5 za kukaa ardhini, zao hili unaweza kulima mara  4  mwaka. Mfano ukiwa na  ekari 5  kila eka moja inaweza kukuingizia Milioni 2 hadi 3.

Mambo muhimu
  • Nafasi inayotakiwa  ni 2mm toka mmea mmoja kwenda mwingine
  • Kila shimo unaweza weka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2 hadi 3 
  • Kila shimo unaweza kupata matunda 4 hadi 6 ( wastani matunda 5).
  • Kwa ukubwa  wa ekari 5 unaweza kuwa na mashimo 1000 hadi 1200
  • Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari (1,000 x 5 x 5 = 25,000)
  • Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 (25,000 x 500 = 12,500,000)
  • Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000
  • Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000
  • Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 Milioni.
Kwa hisani ya Darasa huru

Baadhi ya Njia unazoweza kutumia kupata Wazo Bora la Biashara (Business Idea)


IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIO NAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?

Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kama unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. KUNUNUA FRANCHISE
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE

Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa,Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kazalika

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe
Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kazalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza 

11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

13. TUMIA NJIZA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara- maonyesho ya biashara
Magazeti,
Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
Kwa marafiki

14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako

HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUPATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA

Kwa hisani ya Darasa huru

Site Search